Mimi kwa kweli ni mtoto wa mjini na sikuwa na interest kabisa na mambo ya kilimo. Nakumbuka vizuri kama miaka minne hivi iliyopita babangu (bado alikuwa hai) akiniomba tufanye kilimo wote.
Alikuwa ameanza kupendezwa na kilimo na aliniomba sana. Kiukweli wakati ule nilikuwa na mambo mengi ya mjini na sikuzingatia saana alichokuwa akikisema.
Sikujua kwamba maongezi hayo yangekuwa kati ya maongezi ya mwisho na babangu. Miezi michache baadae aliuguwa ghafla na kupata mauti.
Nilivoenda shamba nilishangaa kuona jinsi alivokuwa amelima hoho, nyanya na spinachi. Shamba lilipendeza sana, na hata tulipata kuuza mazao.
Niliumia sana, kwamba sikuitika wito wa baba alivokuwa hai. Na kwamba sikumuunga mkono kwenye hobby yake mpya.
Basi nilianza kupendezwa na kilimo na nikachukua madarasa ya kilimo. Ili angalau niendeleze ndoto ya babangu.
Hapa Neoland nimejaribu kulima mazao tofauti tofauti. Nilianza na Uyoga (Oyster). Lakini nimelima mapaipai, biringanya, nyanya, maboga ya kizungu, hoho, Chinese, na kadhalika.
Nimekuwa ‘darasani’ kwa kweli. Maana nimejifunza mambo mengi mno. Na kama unavojua darasa la maisha lina gharama.
Ndio sababu nimeanzisha blog hii ilinikunusuru kugharimika kama mimi. Karibuni sana tuelimishane maana elimu haina kikomo.
Pia, Kilimo ni raha!
Ackland Mhina (aka Av)