Faida 5 za Kula Uyoga wa Oyster ni Zipi? Uyoga upo kundi la fungi na sio mboga. Kwa sababu hiyo, uyoga una vitamini na virutubisho vingi zaidi kuliko mboga. Uyoga una madini ya Potasiamu, Chuma, Kopa, Phosphorus na vitamini kama vile B2, B3, B5, B6 na B Complex.
Hii inamaanisha kuwa uyoga una faida nyingi sana kwa afya yako, kwa sababu virutubishi hivi vina imarisha kinga na kupambana na maradhi.
Isitoshe mboya ya uyoga ni tamu sana, kwanini usiiyongeze kwenye dieti yako?
Makala hii itazungumzia faida 5 za kula Uyoga wa Oyster ni Zipi?
Kuna aina nyingi za uyoga, leo tutaangazia aina ya uyoga wa Oyster. Hii ni kwa sababu Uyoga wa Oyster unalimwa sana hapa Tanzania, kwa hiyo upatikanaji wake ni rahisi. Hata wewe unaweza kuanza kulima hapo nyumbani kwako.
- Wingi wa Virutubisho
Kama tulivosema hapo awali, uyoga una fiber,vitamini, madini na virutubisho vingi. Aidha, uyoga wa Oyster una kiwango cha chini cha wanga, kwa hivyo ni chaguo nzuri kwa watu wanaofuata mitindo duni ya lishe. Uyoga pia una kiasi kidogo cha virutubisho vingine, pamoja na vitamini D, madini ya Zinki, na madini ya Seleniamu.
Madini ya Selenium husaidia kushawishi mfumo wa afya mwilini katika kupambana na wadudu wavamizi kama vile bakteria, virusi na fangasi. Lakini pia madini ya Zinki ni muhimu sana katika kutibu vidonda kwa haraka, na kupambana na vimelea vya magonjwa na kuondoa seli zilizo kufa katika mwili.
- Kupambana na kipanda uso (migraine)
Vitamini B2 tuliyoitaja hapo juu ni tiba tosha kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kuumwa kichwa upande mmoja maarufu kama ‘migraine’ yaani kipanda uso. Vitamini hiyo inapunguza kasi ya kuumwa kichwa hicho.
- Inasaidia afya ya Moyo
Uyoga wa Oyster huweza kukuza afya ya moyo kwa kupunguza magonjwa hatari ya moyo kama lehemu (cholesterol) na shinikizo la damu. Hiyo ni kwa sababu uyoga huondoa lehemu iliyoko kwenye moyo na kupambana na shinikizo la damu. Wingi wa protini iliyopo katika uyoga, husaidia kuyaunguza mafuta ya lehemu yaliyotengenezwa na mwili na hatimae kuweka uwiano sawa wa mafuta yanayohitajika katika mwili. Lakini pia uyoga hufanya damu kuwa nyepesi na hivyo basi kurahisisha mzunguko wake mwilini.
- Inaweza kukuza udhibiti wa sukari ya damu
Uyoga wa oyster una faida pia ya kudhibiti ukuaji wa sukari ya damu. Uchunguzi kwa watu walio na kisukari wamegundua kuwa uyoga wa Oyster unaweza kuboresha viwango vya sukari kwenye damu na mambo mengine ya kiafya yanapochukuliwa kama nyongeza au inapotumiwa kama sehemu ya lishe.
- Uyoga wa Oyster unaweza kupunguza hatari ya saratani
Uyoga una chembechembe inayopambana na sumu na kemikali ambazo zinaweza kuathiri seli za mwili wako. Hii inasaidia kuua seli za saratani ambazo zinatengenezwa mwilini na kusababisha saratani.
Madaktari wanaendelea kufanya majaribio lakini uchunguzi wao hadi sasa unaonekana kuwa na matokeo ya kupunguza hatari ya saratani.
Hizi ndio faida 5 za kula Uyoga wa Osyter. Je unafahamu jinsi ya kutungeneza? Utengenezaji wake ni wa rahisi sana. Katika makala ijayo tutazungumzia njia tofauti za kupika uyoga wa Oyster.
Makala hii ilisema faidi 5 za kula Uyoga lakini tutakuongezea faidi zingine 2 za kula Uyoga katika maisha yako.
6. Msaada wa Uzito
Sisi ambao tunaogopa kula nyama kwa wingi halafu tuanza kupata kitambi basi,Uyoga wa oyster ni chakula cha chini cha kalori na mafuta, hivyo ni chaguo bora kwa wale ambao hawataki kunenepa.
Pia, nyuzi zilizopo kwenye uyoga hawa zinaweza kusaidia kutoa hisia kamili na kudhibiti hamu ya kula.
7.Chaguo kwa Lishe ya Mboga
Uyoga wa oyster ni chaguo bora kwa watu wanaofuata lishe ya mboga au lishe isiyo na nyama. Wanatoa protini na virutubisho vingine muhimu ambavyo vinaweza kusaidia kujenga na kudumisha afya bora bila kutegemea nyama.
Natumaini umefaidika na makala hii. Kama una swali lolote tafadhali wasiliana na sisi kupitia whatsapp au telegram hao chini.
Unataka kufahamu jinsi gani ya kulima uyoga? Soma makala hii.
Image by beauty_of_nature from PixabayPicha kutoka kwa My Pure Plants