Ackland Mhina

AVM CS Vertical-FINAL

Jina langu ni Ackland Mhina au unaweza kuniitaa AVM, unaweza kuniita Mkulima Mdogo. Nilianza kulima tangu mwaka 2020 baada ya mzee wangu(Benjamin Mhina) kuongelea sana kwa hisia nyingi na hasa kuona amelima kwenye Shamba lake. Mzee wangu alikuwa amelima Chinese, Hoho na Nyaya.

Nilivutiwa sana na jambo hilo na nilivyoona furaha na amani alikuwa nayo. Kifo kilimkuta na kuacha shamba lake na mimi hapo ndo nikaanza kufanya hiyo shughuli ya kilimo. Kilimo hakikuwa rahisi lakini ninakipenda sana na kimenifundisha mambo mengi.

Mtandao huu utakuonyesha safari ambayo mimi mwenyewe nimepitia. Makala zitaonyesha aina mbalimbali ya kilimo nilichofanya na matokeo yake.

Natumaini utajifunza na wewe pia kuanza kilimo au hata bustani yako ndogo nyumbani. Karibu Neoland Farms.