Hatua 5 za kupanda Strawberry Nyumbani. (Makala iliyopita tuliona faida za strawberry mwilini.)
Makala hii ni moja ya mfululizo wa kukonyesha hatua hizo. Makala hii itakuwa kukuonyesha hatua za mwanzo za matayarisho.
Hatua 5 za kupanda Strawberry Nyumbani. Hizo Hapo
1.Tafuta containers kama hizo unaziona hapo chini. Hizi container zinauzwa 1,500 kila moja.👇
2.Toboa chini. Picha ya hapo chini inaonyesha matobo mangapi yanayotakiwa, idadi inaweza kuwa kuanzia 6-8 kila container.👇
3.Tafuta mchanga mzuri. Tafuta mbolea ya mavi ya ng’ombe.
4.Utanza kuchanganya kwanza mchanga huo na mbolea ya mavi ya ng’ombe kidogo. Baada ya hapo utatoa mche wako uliopata na kuweka kwenye container lako.
5.Tafuta maranda ya mbao ambayo itasaidia strawberry zikitoka zikae vizuri.
Notes:
Usisahau kumwagia maji baada ya kupanda.
Unaweza kumwagia maji kidogo tu mara moja kwa siku. Ukiwa kikombe cha chai, nusu kikombe hicho ukiweka maji na umwagie kila siku. Strawberry zinapenda mchanga wake na mbolea ziwe nyevunyevu kidogo na sio sana. Picha ya hapo chini inaonyesha jinsi inavyotakiwa kuwa 👇
Hivyo ndivyo jinsi ya kupanda strawberry nyumbani.
Makaka ya pili tutaona jinsi ya kutunza strawberry nyumbani. Changamoto ambazo mimi nilipitia na jinsi ngani ya kukabiliana nazo.
Natumaini umefurahia sana makala hii, kama umefurahia naomba utachie comment hapo chini. Je, ungependa kupanda strawberry hapo nyumbani kwako?