Tunda la Strawberry lini Faida zipi 5? Kabla kuongea kuhusu faida hizo 5 za strawberries katika mwili wako, tuanze kwanza na kufahamu strawberries nini?
Table of Contents
Strawberries ni Nini?
Strawberries au kwa jina lingine Fragaria ni moja ya familia ya maua aina ya rose(rosaceae) na moja ya tunda la beri ambalo linajulikana zaidi duniani. Aina za strawberries ziko zaidi ya 10 ambazo zina tofautiana kwa utumu, ukumba na umbo.
Strawberry sio tunda kwa sababu linaweka mbegu zake nje na linaza watoto ambao hao watoto wanatoa mizizi. Mizizi hiyo baadae inakuwa mmea na kuanza kutoa strawberries zingine.
Ukipenda kufahamu jinsi ya kuongeza miche mingine ya strawberries kutumia runners tafadhali soma makala hii kwa kubonyeza hapa.
Tuona Tunda la Strawberry lini Faida zipi 5?
- Kulinda Moyo Wako
Strawberries zinakuwa na aina ya vichembechembe vinavyoitwa anthocyanidins. Hivi vichembechembe vinasaidia na kupunguza mshtuko wa moyo na shinikizo la damu pia. Moyo wako utashukuru sana ukiendelea kula strawberries kila wakati. Hiyo ndo faida ya kwanza.
- Kufukuza Mafua
Strawberries zimejaa vitamins nyingi sana. Mfano ukila strawberries 5 tu kwa siku utakuwa umeongeza 98% ya vitamin C kwenye mwili wako. Vitamins C itasaidia kujenga mfumo wa kinga kwenye mwili wako. Ukifanya hivyo utasaida kupunguza magonjwa madogo kama mafua na kuweza kupona haraka zaidi.
- Kumsaidia Mwanamke akiwa Mjamzito
Mara nyingi mwanamke akiwa mjamzito anashuruwa kula vyakula ambavyo vina virutubisho aina ya folate au asidi ya folic ilikuweza kumsaidia mtoto aliyetumboni kukua vizuri. Tunafurahi kuwajulisha kuwa strawberry ina virutubisho aina ya folate au asidi ya folic. Ukila strawberry itakuwa halisi na kikombe kimoja cha beri kina 40 micrograms ya folate.
- Kuboresha Usagaji Chakula
Utakuwa unafahamu kuhusu fiber(nyuzinyuzi) ambazo zinaleta virutubisho kwenye mwili wako. Strawberries zimejaa fiber(nyuzinyuzi) ambazo zinasaidia usagaji wa chakula kwenye mwili wako. Pia strawberries zinakuwa na maji maji ambayo pia inasaidia kwenye mfumo wa kusaga chakula na kusaidia katika kuvimbiwa na tumbo.
- Kudhibiti Sukari ya Damu
Strawberries zina asilimia ya chini ya glycemic kuliko matunda mengine. Strawberries itasaidia kwenye kudhibiti sukari ya damu. Utafiti mbalimbali umeonyesha kuwa kula strawberries kila siku kutapunguza sana aina ya magonjwa kama kisukari.
Natumaini swali lako la je unafahamu faida 5 za strawberry kwenye mwili wako limejibiwa. Faida za strawberry zipo nyingi sana, acha tukuongezee faida mbili zingine ambazo ni muhimu pia.
- Kupunguza Uvimbe
Asidi ya ellagic, ambayo hupatikana katika strawberries, inaonyeshwa kuwa na uwezo wa kupunguza uvimbe mwilini. Uvimbe wa kibaiolojia unahusishwa na magonjwa mengi kama vile saratani, ugonjwa wa moyo, na magonjwa ya autoimmune. Kwa kula strawberries, unaweza kuchangia kupunguza hatari ya magonjwa haya kwa kuzuia uvimbe wa kimetaboliki na kinga.
- Afya ya Akili
Flavonoids katika strawberries zinaweza kusaidia kudumisha afya ya akili kwa kuongeza mzunguko wa damu kwenye ubongo na kusaidia kuzuia kupungua kwa kazi ya akili. Kwa kufanya hivyo, hizi flavonoids husaidia kuongeza hewa safi na virutubisho kwa ubongo, na hivyo kusaidia kuimarisha kazi za utambuzi na kuzuia kupungua kwa kazi ya akili unapokuwa na umri.
- Usimamizi wa Uzito
Strawberries zina kalori kidogo na mafuta kidogo, lakini zina ladha tamu, hivyo zinaweza kuwa sehemu muhimu ya lishe ya kupunguza uzito. Strawberries ni chanzo kizuri cha nyuzi na maji, lakini ni chini katika kalori na mafuta. Hii inamaanisha kwamba unaweza kula idadi kubwa ya strawberries bila kuongeza kiasi kikubwa cha kalori kwenye lishe yako.
Nyuzi husaidia kutoa hisia ya kujazwa na kudhibiti hamu ya kula, na maji yaliyomo katika strawberries yanaweza kuchangia unywaji wa maji ya kutosha, ambayo ni muhimu katika kudumisha uzito unaofaa.
Ukiulizwa Tunda la Strawberry lini Faida zipi 5? Sasa unaju angalau faida hizo 5. Pia na wewe mtu akikuliza Tunda la Strawberry lini faida zipi 5? Pia unaweza kumjibu mtu huyo.
Ukipenda kutufahamisha faida zingine tafadhali tuandikie comment yako hapo chini. Neoland Farms tunajitahidi sana kufanya utafiti kwa ajili ya kuwasaidi watu wote wawena afya nzuri.
Unafahamu unaweza kutengeneza juice au smoothie ya strawberry. Makala hii inaeza jinsi ya kutengeneza smoothie tamu sana ambayo unaweza kutengeneza hata nyumbani kwako.
Picha ya Engin Akyurt kutoka Pixabay