Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

Coriander ni mmea ambao unaleta ladha nzuri kwenye chakula. Leo tutaona jinsi ya kupanda coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1.

Katika mmea ambayo ni lazima kupanda nyumbani kwako ni Coriander. Ukipenda kujua faida za Coriander tafadhali somo makala hii.

Kwa vile ninaishi mjini kwenye magorofa na sina sehemu ya kupanda mazao. Njia rahisi ni kupanda kutumia Kontena. Njia hii ni rahisi na haina gharama kubwa.

Mara nyingi kwenye mtandao wetu, hasa sehemu ya sehemu ya Bustani tunaongelea sana jinsi ya kupanda kwa kutumia Kontena.

Ilikuwa tarehe 4/8/2024 ndo nilipanda mmea wa Coriander kwenye Kontena. Nyumbani tunapenda sana kutumia Coriander hasa tukipika nyama ya aina yote. Sababu hiyo kuleta ladha katika chakula hicho au mboga hiyo.

Kama wewe haupendi kula maharage au unapenda kula, jaribu kuongeza Coriander kwenye maharage. Mwenye utaniambia matokeo yake.

Siku zote tunanunua fungu la Coriander kwenye soko kuu la Kisutu kwa Buku Tu. Mara nyingi hatumalizi hilo fungu. Lakini nikasema acha tujaribu kupanda.

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1.

Fuata hizi hatua baada ya hatua na ukiangalia picha hapo chini pia

1.Kwanza nilichukua Kontena ya maji makubwa ya lita 13.👇

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

2.Nilichanganya udongo pamoja na Mbolea ya Samadi na kuweka kwenye Kontena hizo.

3.Nilitengeneza mashimo wa mawili na kuweka mbegu moja kwenye kila shimo.👇

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

4.Nilifunikia na udongo, kisha nikamwagilia maji.👇

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

Hivi ndivyo nilivyopanda Coriander kwenye Kontena.

Je kupanda kwenye Kontena kulifanikiwa? Hapana. Mbegu ambazo nilipanda hazikutoka kabisa. Nilisubiri kwa wiki kadhaa.

Nilikata tamaa kweli. Baadae nilijipa moyo na kujaribu nyia nyingine. Nilipanda kwenye Kontena tofauti.👇

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

Kwenye Kontena hizi niliweka mashimo 8 kwa sababu lilikuwa kontena lenye upana mkubwa. Mashimo hayo 8 niliweka mbegu mbili mbili badala ya kuweka mbegu moja moja kama nilivyofanya mara ya mwisho, sababu ya kufanya hivyo nikuweka asilimia kubwa kwenye mbegu moja iweze kuzaa.👇

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

Kwa hiyo kila mwezi nitakuwa nikisasisha(update) maendeleo ya jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena.

Sasa tuone mambo mengine ambayo ni muhimiu kama faida za kupanda kwenye Kontena na hata pia mambo ya kuzingatia wakati wa jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1.

Faida za Kupanda Coriander kwenye Kontena

Kupanda coriander kwenye kontena kuna faida nyingi. Kwanza, itakusaidia kudhibiti mazingira ya ukuaji wa mimea. Unaweza kudhibiti ubora wa udongo, jinsi ya kumwagia maji, na mwanga wa jua kwa urahisi zaidi. 

Hii ni faida kubwa kwa wale wanaoishi kwenye miji mikubwa au maeneo yenye nafasi ndogo za bustani kama mimi😃. Kwa kuwa coriander ni mimea inaokua kwa muda mfupi, unaweza kuvuna mara kadhaa msimu mmoja ikiwa matunzo yake ni mazuri.

Jinsi ya kupanda Coriander kwenye Kontena-Sehemu ya 1

Faida nyingine ni uwezo wa kuhamisha mimea kirahisi. Kontena linaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na hali ya hewa au mwanga wa jua. Ikiwa kuna mabadiliko ya hali ya hewa ghafla, unaweza kulinda mimea yako kwa kuiweka ndani ya nyumba au eneo lenye kivuli.

Mambo ya Ziada ya Kuzingatia

Pia, kumbuka kwamba coriander inahitaji mwanga wa kutosha wa jua. Hakikisha kontena limewekwa mahali penye mwanga wa jua kwa angalau saa sita kwa siku. Kama utapanda coriander ndani ya nyumba, unaweza kutumia taa maalum za kukuzia mimea ili kuhakikisha inapata mwanga wa kutosha.

Kwa kumalizia, upandaji wa coriander kwenye kontena ni njia nzuri ya kujiweka karibu na mimea yako na kuwa na uhakika wa ubora wa mazao yako. Ikiwa una nia ya kuongeza ujuzi wako zaidi kuhusu upandaji kwenye kontena, hakikisha unaendelea kufuatilia makala zetu zijazo.

Basi uwe ukitembelea mtandao wetu na kuona maendeleo hayo. Pia tunapendekeza kuendelea kuangalia njia zingine za kupanda mbogamboga kwenye Kontena.

Kama umefaidika na makala hii tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Tutakuwa na hamu ya kusikia maoni yako. Pia tunaomba tueleze kama tayari umeshawahi kupanda zao lolote kwa kutumia njia ya Kontena au ndo unataka kuanza kupanda.

Basi mpaka wakati mwingine endelea kupanda, kulima na kufurahia kwa sababu Kilimo kiwe kidogo au kikubwa Kilimo ni Raha!!

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these