Ona jinsi nilivyopanda mbegu 2 za Nyanya Tofauti. Kabla sijawaambia nilivyofanya lazima niwaambie kwa nini niliamua kufanya hivyo.
Wiki mbili kabla ilikuwa tarehe 12/7/2024, nilipanda mbegu kwenye kontena dogo nikifikiria kuwa Nyaya hizo zitakuwa na kuota Nyanya. 👇

Baadae niliona kuwa nimefanya kosa. Kosa hilo lilikuwa ni kupanda kwenye kontena dogo na ukuaji wa mmea ungekuwa tatizo baadae. Pia Nyanya hizo zingekuwa na uzito. Kontena dogo hilo lisingeweza kustahimili uzito huo.

Nilitafakari na kupata wazo. Nikasema nitapeleka Nyanya hizi shambani nakuamishia huko. Wiki mmoja baadae nilikuwa shambani.
Ndugu yangu mmoja anayeitwa masanilo alikuwa na mbegu nyingi tofauti na ambayo nilikuwa nazo.
Wazo likaja kwa nini nisipande mbegu 2 za Nyanya Tofauti. Huko shamba nilikuwa na madumu ya kontena za maji. Sasa acha niwaonyeshe jinsi nilivyopanda mbegu 2 za nyanya tofauti.
1. Madumu ya Kontena za Maji ya lita 13– Nilichukua madumu haya mawili nikayakata nusu. Dumu mmoja nilipanda Mbegu ya aina mmoja na dumu la pili nilipanda aina nyingine.

Nilichanganya udogo pamoja na mbolea ya ng’ombe na baada ya hapo kuzipanda hizo mbegu. Mbegu hizo nilipanda tarehe 22/7/2024.

Mwezi mmoja na nusu umepita sasa. Mbegu ambayo imetoka ni ya kampuni mmoja. Mbegu ya kampuni nyingine imekubali.

Tutaanza kufuatilia mbegu hii ambayo imekubali na kukupa habari kila mwezi na jinsi inavyoendelea mpaka pale tutapopata mavuno yetu.
Kipindi kimepita sasa na zoezi hili haikufanikiwa. Soma ni nini? Nimejunza kuwa ni vizuri kupanda mbegu nyingi za aina hizo mbili badala ya kupanda miche michache.
Zoezi nyingine nitafanya hivi karibu la kupanda nyanya kwenye Kontena za Plastic na tutaona. Makala hiyo tutaweka hapa kwenye tovuti yetu.
Ukipenda unaweza kusoma baadhi ya makala kuhusu kilimo kwenye page hiyo ya kilimo.
Mpaka wakati mwingine
Mimi ni AVM