Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Hatua 3 za kupanda passion kwenye sehemu ndogo. Nilikuwa natafuta tunda la kupanda. Dada yangu mmoja akaniambia kwa nini usijaribu kupanda zoa la Passion. Dada huyo alinipata sababu kadhaa ambazo zilinivutia kupanda.

Safari ilianza mwaka 2023 mwezi wa pili tarehe 27. Nilinunua miche kadhaa kama unavyoona kwenye picha hapo chini.👇

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Hatua 3 za Kupanda Passion Kwenye Sehemu Ndogo.

1. Tafuta Mche Bora wa Passion Fruit.

Kama nilivyosema awali nilinunua miche kadhaa  lakini nilinunua pia kutoka sehemu mbili tofauti.

Sababu ya kufanya hivi ni kuona miche ipi itazaa matunda mengi na ipi haitazaa kabisa. Niliweza kujua baadae kabisa na kujifunza mambo mengi.

2. Kuchimba Mashimo ya Ukubwa wa Kiasi

Miche ya Passion inakuwa kwa urefu na pia chini inasamba, kwa hiyo inahitaji nafsi nzuri. Nafasi hiyo itasaidia hata wakati wa kuweka dawa au mbolea iwepo. 👇

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

3. Nunua Vifaa Vinavyofaa.

Ninamaanisha nini kununua vifaa vinavyofaa? Vifaa vinavyofaa ni kama:

(a) Mbolea ya Ng’ombe

(b)Mirunda ya Mbao

(c)Kenchi Wire

Vifaa hivi vitasaidia na mambo mengi.

Mfano: Mbolea ya Ng’ombe itasaidia na ukuaji wa mche huo. Kwa msaada wa dada yangu tuliweza kuweka mche sita. Tulichimba mashimo makubwa na kuweka mbolea nyingi ya ng’ombe na kupanda mche miwili katika kila shimo.👇

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Mirunda ya Mbao kazi yake ilikuwa ni kusimamisha hiyo mche baada ya kukua kwa urefu flani.👇

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Kenchi Wire kazi yake ni kusaidia mche huo usambae vizuri kabisa. Pia kumbuka Passion Fruit zikianza kuzaa huwa zina uzito kidogo kwa hiyo unahitaji kenchi wire.👇

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Matunzo ya Passion Fruit:

Passion Fruit haina matunzo makubwa sana. Jambo la muhimu ni kumwagia maji kila siku bila kukosa. Unaweza kumwagia maji hata mara mbili kwa siku kama ni msimu wa joto.

Upande wa magonjwa, passion fruit sio zao ambalo linapata magonjwa kabisa. Tangu nianze kupanda au kulima sijawahi kupata magonjwa. Nilipiga dawa ya magonjwa mara moja tu na hiyo ni kwa sababu nilikuwa na piga dawa mazao mengi nikaamua kipiga na passion fruit.

Utunzaji wa passion fruit hauna kazi kubwa sana. Jambo kubwa ni UVUMILIVU WAKO TU. Ukipanda zao hili la Passion Fruit kama zao jingine lazima uvumilie mpaka uanze kuona mazao yake.

Changamoto za kupanda Passion Fruit kwenye Sehemu Ndogo:

Kupanda passion fruit (matunda ya pasi) kwenye sehemu ndogo kunaweza kuleta changamoto kadhaa. Hapa kuna changamoto kuu ambazo unaweza kukutana nazo na nyingine nilikutanana nazo kama Nafasi Ndogo, Mwanga wa Kutosha, Udhibiti wa Magonjwa na Wadudu, Matumizi ya Maji na Mbolea, Upandaji wa Mimea Mingi na Mzunguko wa mazao.

Hizi ndo zilikuwa kuwa changamoto za kupanda Passion kwenye sehemu ndogo.

Changamoto mmoja ambayo niliona ni hii hapa Matumizi ya Maji na Mbolea

Upungufu wa maji: Katika maeneo madogo, inaweza kuwa changamoto kudhibiti kiasi sahihi cha maji, kwani udongo unaweza kukauka kwa haraka au kujaa maji. Passion fruit inahitaji udhibiti mzuri wa unyevu ili isiharibike.

Mbolea na virutubisho: Mimea ya passion fruit inahitaji virutubisho vya kutosha kama potasiamu, fosforasi, na nitrojeni. Eneo dogo linaweza kuhitaji matumizi sahihi ya mbolea ili kuhakikisha mimea inapata virutubisho vya kutosha.

Vipi kuhusu faida za kupanda Passion Fruit kwenye Sehemu Ndogo? 

Hizi hapa ndo baadhi ya faida zake. Faida ya kwanza ni Matumizi Bora ya Nafasi, Uzalishaji Bora wa Matunda na Urahisi wa Kudhibiti Magonjwa na Wadudu.

Faida moja kubwa ambayo nilipenda kuhusu kupanda passion kwenye sehemu ndogo ni Matumizi Mbalimbali ya Passion.

Matumizi ya matunda: Matunda ya passion yanaweza kutumika kutengeneza juisi, jam, desserts, na pia hutumiwa katika mapishi mengine mengi. Hii inaongeza thamani na ubunifu kwenye matumizi ya mazao ya nyumbani.

Hizi ni baadhi tuu ya faida za kupanda Passion Fruit kwenye sehemu ndogo. Ukipenda kufahamu changamoto na faida zake kwa undani zaidi bonyeza hapa.

Hatua 3 za kupanda Passion kwenye Sehemu Ndogo.

Kufahamu zaidi kuhusu mambo niliyojifunza baada ya kupanda Passion Fruit tafadhali bonyeza hapa.

Natumaini umefurahia kufahamu hatua 3 za kupanda Passion Fruit kwenye Sehemu Ndogo. Kama umefurahia makala hii basi unaweza kusoma makala zingine kwenye mtandao wetu.

Mpaka wakati mwingine. Kilimo Ni Raha!

Picha zimepunguzwa na website ya Image Resizer.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these