Leo nitawaonyesha hatua 5 za kupanda kitunguu Saumu kwenye Kontena. Nilinunua aina ya garlic yenye mbegu kubwa kwenye soko la Kisutu. Unaweza kupata Garlic kwenye soko lililo karibu nawe. Nikaamua kupanda kwenye kontena hiyo hapo chini.👇

Nilipanda hizi garlic tarehe 9/8/2025.
Kwa hiyo kwenye makala hii nitakuonyesha hatua kwa hatua na ili wewe pia uweze kupanda nyumbani kwako. Ukipenda mwenyewe utafurahia na utakuwa na afya bora. Sasa tuone hizo hatua 5 za kupanda kitungu saumu kwenye kontena.
1. Kontena inayofaa.
Upande wa Kontena ni vizuri kuwa na kontena kubwa. Kontena za maji kama za Lita 13 au Lita 20 ni nzuri. Unaweza kukata nusu kwa njia mbili tofauti, kama picha inavyoosha hapo chini.👇

2. Changanya Udongo na Mbolea.
Udongo wako hakikisha ni udongo laini na mzuri, hauna mbwembwe. Halafu baada ya hapo unaweza kuchanganya udongo huo na mbolea ya ng’ombe. Baada ya kuchanganya mimi napenda kuacha angalau siku mbili au tatu.(pendekezo sio lazima).
3. Tayarisha mbegu zako.
Ukinunua kitungu saumu ananza kutoa maganda yake. Hakikisha kitungu saumu zina kuwa kama hivyo, kama picha inavyoosha hapo.👇

4. Panda Kitunguu Saumu kwenye Kontena.
Hapa utachukua Kontena lako baada ya kuzikataa ambavyo unapenda wewe. Kisha kuchukua udongo wako ambao umechanganywa na mbolea ya ng’ombe.
Weka udongo wako kwenye kontena yako. Baada ya hapo tengeneza mashimo kulingana na idadi ya vitungu saumu ulivyopata.
Vitungu Saumu hivyo hakikisha kwenye kitako ndo kipo chini unapoweka kwenye shimo lako. Baada hapo fikia, fanya hivyo kwenye mashimo yote yenye vitungu saumu. Ukimaliza kufanya hivyo mwangia maji.👇

5. Matunzo
Kila baada ya siku moja unamwangilia kontena zako. Baada ya wiki moja utaona kitungu saumu ulichopanda kinaanza kuzaa na kutokeza jani.
Baada ya Wiki 3–4 kitungu saumu kuota unaweza kuweka mbolea yenye nitrojeni kidogo (mfano DAP, au mbolea ya mboji + majani yaliyooza). Hii husaidia majani kukua vizuri.
Sasa utasubiri kidogo kama mwezi halafu mwezi wa 2–3 utaongeza mbolea yenye phosphorus na potashi (mfano NPK 17:17:17 au 23:23:0). Hii husaidia mizizi na kutengeneza vitunguu vikubwa.
Mwezi wa 4 kwenda 5 ukifika utaacha kuongeza mbolea nyingi ili visipate majani mengi kupita kiasi badala ya vitunguu.
Kuhusu magonjwa ambayo unaweza kupata wakati unapanda kitungu saumu ni madogo sana kuliko shambani, lakini ni vizuri kuwa kinga. Ukipata ukungu (fungus) mara nyingi inapatikana kwa sababu ya maji mengi. Tumia dawa za kikaboni kama sulphur au copper fungicide mara moja kwa mwezi, au tumia dawa asilia (kama mchanganyiko wa majani ya neem).
Ukipata wadudu wanaokula majani unaweza kutumia dawa ya majani ya mwarobaini (neem) au maji yaliyochemshwa ya vitunguu + pilipili kali (spray asilia).
Hizo ndo hatua 5 za kupanda Kitungu Saumu kwenye Kontena. Basi nitakuwa na sasisha(update) kuona maendeleo ya Kitungu Saumu kwenye Kontena.
Natumaini umefurahia makala hii. Hapa kwenye Neoland Farms tunajitahidi kukupa makala ambazo zitakuchochea kuchukua hatua za kupanda mazao mbalimbali. Tutakuonyesha mazao ya aina mbalimbali ambayo unaweza kupanda hapa hapo nyumbani na hata pia kama unasehemu ndogo ya kupanda mazao.
Je, umeshawahi kupanda kitungu saumu? Je, wewe ni mtumiaji wa kitungu saumu wa kila siku? Je, unafahamu baadhi ya mafua ya kitungu saumu? Basi naomba tuambie kwenye sehemu ya comment hapo chini. Ukipenda kufahamu mengi kuhusu mazao mbalimbali soma ukurusa wetu wa Je, Wajua?
Neoland Farms tupo tayari kukushika mkono na kukuonyesha kwa picha na hata video jinsi ya kupanda mazao mbalimbali. Unaweza kuangalia ukurusa wetu wa bustani au hata kilimo na ujionee mwenyewe jinsi gani tumeweza kupanda mazao tofauti na pia kuandika changamoto ambazo tumepitia sisi wenyewe. Sisi kwa kufanya hivi tunakusaidia kuelewa mapema na kuruka matatizo hayo, hata kama utapata changamoto zitakuwa ni kidogo.
Mpaka wakati wengine
Mimi ni AVM