Leo tutangalia aina 10 za mmea wa Lavender. Naomba nikuuilize swali. Je, umewahi kujikuta unanusa harufu tamu, laini, na ya kutuliza akili? Harufu hiyo inayoweza kukufanya ujisikie uko katika bustani yenye amani, mbali na pilika za dunia? Kama uweshawahi kuhisi hivyo basi hauko mwenyewe.

Naam, ni harufu gani hiyo? Ni harufu ya Lavender – mmea wenye historia ndefu, uzuri wa kuvutia, na matumizi mengi sana. Leo, nakualika tufanye safari ya kipekee, tuchunguze asili yake, tuone wapi unapatikana, na tugundue aina kumi (10) za Lavender ambazo labda umewahi kuziona au kuzisikia, na zile ambazo zitakushangaza.

Sasa tuone kwanza historia fupi ya mmea huu wa Lavender. Mmea wa Lavender una historia ndefu, tukianzia maelfu ya miaka iliyopita. Neno ‘Lavender‘ linadhaniwa kutoka kwenye neno la Kilatini ‘lavare’, ambalo linamaanisha ‘kuosha’. Hii haishangazi, kwani Wagiriki na Warumi wa Kale waliitumia sana kwenye maji yao ya kuoga, kwa ajili ya kufanya mwili uwe na harufu nzuri na pia kwa ajili ya kutuliza akili.
Tusisahau pia Waingereza, hasa wakati wa Elizabeth I (karne ya 16), waliipenda sana mpaka kuitumia kama dawa ya kusafisha nyumba na pia kama manukato. Ilikuwa maarufu sana kwa sababu ilisaidia kufukuza nzi na wadudu wengine. Fikiria jinsi ambavyo mimea hii midogo imeweza kuingia kwenye historia na tamaduni za ulimwengu, ikitumika kwa ajili ya afya, uzuri, na hata katika ibada za kidini!
Lavender ni mmea unaostawi katika hali ya hewa ya Mediterania – yaani, joto na ukame. Eneo la asili la mmea huu ni kwenye:
Hata hivyo, kutokana na umaarufu wake, Lavender sasa inalimwa kibiashara na kibinafsi ulimwenguni kote. Tunaiona inalimwa Marekani (hasa Oregon na Washington), Australia, Bulgaria, na hata katika baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki, ambapo hali ya hewa imerekebishwa kuendana na mahitaji yake. Bulgaria kwa sasa inajulikana kuwa ni moja ya wazalishaji wakubwa wa mafuta ya Lavender duniani.

Ulimwengu wa Lavender ni mpana sana kuliko tunavyofikiria! Unajua kuna zaidi ya aina 45 (spishi) za Lavender, na mamia ya mimea iliyoboreshwa (cultivars). Lakini tutazungumzia aina 10 za mmea wa Lavender ambazo zitakupa picha kamili ya utofauti wake:
| Namba | Jina la Kisayansi (Spishi) | Jina Maarufu | Inapatikana Wapi (Asili/Uzito wa Uzalishaji) | Sifa za Kipekee |
| 1 | Lavandula\ angustifolia | English Lavender (Lavender ya Kiingereza) | Ulaya (Ufaransa, Bulgaria, Uingereza) | Inajulikana kwa harufu yake nzuri na utamu. Ndiyo chanzo kikuu cha mafuta ya Lavender ya hali ya juu. Hutumika sana kwenye upishi. |
| 2 | Lavandula\ latifolia | Spike Lavender | Hispania, Ufaransa, Italia | Inatoa harufu kali zaidi, yenye ‘kemfora’ (camphor), si tamu sana. Mafuta yake hutumika sana katika matibabu ya nje (liniments) na usafishaji. |
| 3 | Lavandula\ x\ intermedia | Lavandin (Mseto) | Ufaransa (Provence), Marekani, Australia | Ni mseto wa No. 1 na No. 2. Inatoa mafuta mengi kuliko yote, kwa hiyo inalimwa kibiashara. Harufu yake ni tamu na yenye kemfora. |
| 4 | Lavandula\ stoechas | Spanish Lavender (Lavender ya Hispania) | Hispania, Ureno, Kaskazini mwa Afrika | Inajulikana kwa maua yake ya kipekee yenye ‘masikio’ au ‘mabawa’ juu. Harufu yake inaweza kuwa kama kemfora au resini. Hupandwa zaidi kwa ajili ya urembo. |
| 5 | Lavandula\ dentata | French Lavender (Lavender ya Ufaransa) | Bahari ya Mediterania, Kaskazini mwa Afrika | Majani yake yana umbo kama meno (dentata), ndiyo maana imepewa jina hilo. Harufu ni nyepesi na ya mimea (herbal). Huweza kustahimili baridi kiasi. |
| 6 | Lavandula\ multifida | Fernleaf Lavender | Visiwa vya Canary, Kusini mwa Hispania | Majani yake yanafanana na majani ya ‘fern’ (jani la upanga). Inastawi kwenye hali ya hewa ya joto na inatoa maua mara kwa mara. Harufu yake ni ya viungo(spicy). |
| 7 | Lavandula\ lanata | Woolly Lavender | Hispania | Imefunikwa na nywele nyeupe, na kuifanya ionekane ‘woolly’ (kama sufu). Hii huisaidia kustahimili ukame mkali. Harufu yake ni kali. |
| 8 | Lavandula\ viridis | Green Lavender (Lavender ya Kijani) | Madeira, Visiwa vya Canary | Ni ya kipekee kwa sababu majani na maua yake ni ya kijani-njano. Inatoa harufu kali ya limau au machungwa. |
| 9 | Lavandula\ pedunculata | Fringed Lavender | Hispania, Ureno, Moroko | Inafanana na Spanish Lavender (No. 4) lakini ina shina ndefu zaidi. Maua yake yanaonekana kama kofia ndogo juu ya shina refu. |
| 10 | Lavandula\ heterophylla | Sweet Lavender (Lavender Tamu) | Mseto wa bustani (Garden Hybrid) | Ni mseto unaojulikana kwa maua yake kuendelea kutoa maua kwa muda mrefu na harufu yake ya kupendeza na tamu (sweet). |
Kama tulivyosema awali kuwa kuna aina 45 za lavender lakini sisi tumeongelea aina 10 za mmea wa lavender kwa siku ya leo. Wakati mwingine tutafanya utafiti wa mmea hiyo 35 iliyobaki.
Sasa, rafiki yangu, tumefahamu historia kidogo pamoja na aina 10 za Mmea wa Lavender. Lakini kuna mambo machache kuhusu mmea huu ambayo wengi wetu hatuyafahamu, je unajua ni yapi hayo?
1. Sio Zote Ni Rangi ya Zambarau: Ingawa tunafikiria Lavender ni lazima iwe na rangi ya zambarau, kuna aina (kama No. 8, Green Lavender) ambayo maua yake ni ya kijani-njano. Pia, kuna aina zinazotoa maua meupe au ya rangi ya waridi (pink).
2. Asali ya Kipekee: Asali inayotokana na nyuki wanaochukua asali kutoka mashamba ya Lavender inaitwa Lavender Honey. Inajulikana kuwa na ladha ya kipekee, yenye harufu nzuri, na tamu sana. Inathaminiwa sana na wataalamu wa asali.
3. Inafukuza Panya na Wadudu: Mbali na nondo (moth), Warumi wa Kale waliamini kwamba kuchoma Lavender kunaweza kufukuza panya. Siku hizi, hupandwa kando ya bustani kama njia ya asili ya kufukuza wadudu kama vile kupe na mbu.

4. Lavender Inatumika Kama Dawa ya Kwanza (First Aid): Mafuta ya Lavandula\ angustifolia (English Lavender) ni mojawapo ya mafuta machache muhimu ambayo yanaweza kutumiwa moja kwa moja kwenye ngozi bila kutumiwa na mafuta mengine. Inaaminika kuwa inasaidia kutuliza haraka maumivu ya kuungua kidogo, kuumwa na wadudu, na mikwaruzo midogo.
5. Kemikali Zinazotofautisha Aina: Aina kuu mbili, English Lavender (No. 1) na Spike Lavender (No. 2), hutofautiana sana kimatibabu na kunukia kwa sababu ya kemikali zake kuu. English Lavender ina kiasi kikubwa cha Linalool na Linalyl Acetate (zinazopunguza maumivu na kutuliza), wakati Spike Lavender ina kiasi kikubwa cha 1,8-Cineole na Camphor (zinazochochea na kusaidia kupumua).
6. Mchango Wake Kwenye Vita Kuu: Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, Lavender ilikuwa ikitumika kama dawa ya kutibu majeraha na vidonda vya askari kwa sababu ya uwezo wake wa kuzuia maambukizi.
Hayo ndo mambo machache ambayo ladha wengine wetu tulikuwa hatufahamu kuhusu mmea Lavender.
Kwa hiyo, rafiki yangu, safari yetu ya kugundua aina 10 za mmea wa Lavender imefikia mwisho wake, lakini ninatumaini imekufungua macho kuona uzuri na kina cha mmea huu.

Kutoka kwenye mabonde ya Provence, ukioga katika maji ya Warumi wa Kale, hadi kwenye chupa yako ya mafuta muhimu nyumbani, Lavender imebeba historia, uzuri, na amani. Si tu mmea wa kupendeza bali ni hazina yenye matumizi mengi sana. Mara nyingine utakaponusa harufu yake, kumbuka hadithi zake na aina 10 za mmea wa Lavender tulizojifunza leo!
Naomba tuambie kwenye makala hii ya Aina 10 ya Mmea wa Lavender ni zipi ambazo unazifahamu na zipi ambazo ulikuwa hauzijui kabisa. Pia ni mambo gani ambayo yamekushangaza kuhusu mmea wa Lavender.
Tafadhali tuambie kwenye comment section hapo chini. Je, ungependa kufahamua mmea mingine kama hii, tafadhali tembelea ukurusa wetu wa Je,Wajua?
Mpaka wakati mwingine mimi ni rafiki yako