Jinsi ya Kuanda Uyoga wa Oyster? Leo nitakueleza jinsi ya kuanda Uyoga wa Oyster. Kuanda uyoga wa oyster wa aina hii ni kama unataka kufanya biashara ya uyoga.
Kwenye makala za nyuma niliongelea kuhusu faida 5 za kula uyoga wa oyster, ukipenda kusoma kuhusu makala hiyo unaweza kubonyeza hapa. Pia kwenye makala tofauti tuliongelea kuhusu jinsi ya kujenga banda la uyonga, pia ukipenda kusoma unaweza kubonyeza hapa.
Table of Contents
Jinsi ya kuanda uyoga wa oyster inategemea na kiwango cha uzalishaji unachotaka kufanya. Mimi nilianza kwa kuanda kiwango kikubwa cha mifuko za uyoga 1500. Hiki ni kiwango kikubwa sana kwa mara ya kwanza. Nilipitia changamoto nyingi na hili niliongelea kwenye makala hii, ukipenda kujua changamoto hizo bonyeza hapa.
Ningekushauri kwa mara ya kwanza unaweza kuanza na mifuko 250-500, kwa sababu gani ninakuambia hivyo?
- Mifuko hii ambayo utaanza nayo itakusaidia kuusoma vizuri uyoga wa oyster.
- Kwenye banda lako kutakuwa na nafsi ya uyoga wako kupumua vizuri.
- Upande wa uzalishaji utafahamu ni kiwango gani ambacho unazalisha kwa wiki mpaka mwezi.
- Utaweza kuzalisha uyoga bila mwezi na haukosa kuuza uyoga kila mwezi kwa mwaka mzima.
Sasa twende kwenye vifaa ambavyo unahitaji kwa ajili ya kuanda uyoga wa oyster.
Jinsi ya Kuanda Uyoga wa Oyster? Ni hivi:
- Maranda ya Mbao
- Makapi ya Miwa
- Pumba
- Mbolea ya Kuku
- Chokaa
- Sukari
- Urea
- Mkaa
- Mbegu za Uyoga wa Oyster.
Hivi ndivyo vitu vinahitajika kwa awamu ya kwanza. Hivi vitu vyote vinachanganywa pamoja kama unavyoona hapo chini kwenye picha na video.👇
Baada ya kuchanganya hivyo vyote unatacha kwa wiki kama moja ilizipate kuchanganyana vizuri na kushikana kikamili zaidi.
Wiki moja ikishapita sasa unaweza kuanda awamu ya pili. Ni vitu gani ambavyo unahitaji ili kuweka kwenye banda lako la uyoga?
- Mfuko wa Nylon
- Cell Tape
- Rababendi
- Kamba ya kuning’iniza
- Nylon Kubwa
- Dettol ya Maji
- Spirit na Pamba
- Wire
- Mapipa(Haya ni kwa ajili ya kuchemshia mfuko hiyo ya uyoga)
- Mabomba ya PVC ya Blue.
- Kuni
Hivi vitu vyote ni muhimu sana. Baada ya ule mchanganyiko uliokaa wiki moja, sasa unaanza kuweka kwenye mifuko hiyo ya Nylon halafu na chemsha kwenye mapipa. Ukimaliza kuchemsha kwenye mapipa unaweka kama unavyona hapo chini kwenye picha kwa ajili ya kupoa. 👇
Utaziacha tena kwa wiki moja halafu baada ya hapo ndo utaanza sasa kuweka mbegu ya oyster ndani ya huo mfuko. Ukishafika kwenye hatua hii utakuwa umemaliza hatua ya kuanda Uyoga wa Oyster.
Makala inayofuatia utafahamu jinsi gani ya kutunza na kuzalisha mpaka unapata uyoga wako wa oyster. Unaweza kubonyeza hapa kusoma hiyo makala.
Natumaini ufaidika na hilo somo. Ukipenda kupata ushauri tafadhali wasiliana nasi kwa kubonyeza hapa.
Pia tuambie hapo chini umeshawahi kula uyoga au kujependa kulima uyoga. Tutafurahi sana kupata maoni yako.
Asante sana kwa kusoma na uwe na siku njema.
Picha ya Ngoc Huy Nguyen kutoka Pixabay