Karibu tena kwenye sehemu ya tatu kuhusu Uyoga wa Oyster. Utunzaji wa Uyoga wa Oyster na Mavuno yake. Leo tutaona jinsi tunaweza kufanya hivyo.
Kufahamu kwanza jinsi ya kupanda uyoga wa oyster tafadhali soma makala hii kwa kubonyeza hapa.
Utunzaji wa Uyoga wa Oyster na Mavuno yake
- Tayarisha na kuweka kwenye mifuko yake
- Funikia midomo yake. Hii itasaidia mbegu kuenea kwenye mifuko na kuzalisha uyoga wa oyster.
Picha ya hapo chini itakuonyesha jinsi ya kufanya hivyo.👇
- Utaacha hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja
- Toa hayo makaratasi na kuanza kumwagilia uyoga wako.
Utamwagilia uyoga wako kama picha hivyo inavyoonyesha na kutumia kifaa hicho.👇
Utamwagilia kwenye mashimo hayo madogo na kama sehemu yako ina joto unaweza ukamwagilia hata pendeni kwenye mifuko hiyo.
- Maji yako unaweza kuchanganya na barafu ili uyoga uweze kuota na kupata mazao mengi. Kama nilivyosema ukiwa unakaa mkoa ambao una joto kali kama Dar es salaam ni vizuri kufanya hivyo.
Mavuno ya Uyoga wa Oyster
Unaweza ukavuna kuanzia kilo1-5 kwa siku. Kilo 1 ya Uyoga inauzwa kuanzia 5000-10,000 za Kitanzania. Ukiuza soko la Wachina utauza kwa 5,000 na sio zaidi ya hapo, lakini ukiwa na soko lako mwenyewe kama ndugu, jamaa na marafiki utauza kuanzia 8,000 mpaka 10,000 kwa siku.
Soko la Uyoga ni nzuri na utapata fedha nyingi ukilifanya kwa usahihi. Uyoga utavuna mpaka miezi 3 mpaka 4, inategemea utunzaji wako tu.
Mambo Matatu niliyojifunza katika utunzaji wa Uyoga wa Oyster na Mavuno yake.
- Ikiwa unaanza kufanya kilimo cha uyoga wa oyster anza na mifuko michache kama mifuko 300 kuliko kuanza na mifuko mingi kama sisi tulivyoanza. Ukianza na mifuko michache utafahamu zao lenyewe na jinsi ya kulishughulikia.
- Sisi tulilima uyoga wa oyster mkoa wa Dar es salaam na kawaida mkoa wetu huu unakuwa na joto sana. Sehemu ambayo kuna joto jingi uyoga unaota kwa shida sana. Ukilima uyoga wa oyster ni vizuri banda lako la uyoga liwe na udongo kwa nje. Udongo unasaidia kuzuia au kuingiza joto ndani ya banda. Ndani ya banda kutakuwa na ubaridi ambao utasaidia uyoga kutoka kwa wingi.
- Soko la uyoga wa oyster lazima ulifahamu vizuri. Tumia vizuri social media kutangaza uyoga kwa watu mbalimbali. Tumia pia fursa hiyo kuwafundisha watu kuhusu manufaa ya uyoga wa oyster katika miili yao. Ukifanya hivyo utapata watu wengi ambao watanunua kwako.
Hayo ndo mambo matatu niliyojifunza katika utunzaji wa uyoga wa oyster.
Natumaini umefarahia kufahamu mambo mengi kuhusu utunzaji wa uyoga wa oyster na mavuno yake. Ukipenda kutuambia mambo gani umependa na kama ungependa kulima uyoga wa oyster, tafadhali tuandikie hapo chini kwenye comment.
Endelea kufahamu mazao mengine ambayo unaweza kulima kwenye shamba au hata nyumbani kwako. Tupo hapa kusaidia.